|
Mama Anna Mgwira mkuu wa mkoa wa Kilimanajaro ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya ESTL akiongea katika hafla fupi ya uzinduzi wa mradi wa kutokomeza ukeketaji wa wanawake katika mkoa wa Singida (KICK FGM OUT OF SINGIDA) unaotekelezwa na shirika ESTL hafla iliyofanyika katika ukumbi wa RC SOCIAL TRAINING CENTRE nakuwakutanisha wadau mbalimabli mgeni rasimi katika hafla hiyo mkuu wa mkoa wa Singida ambaye amewakilishwa na katibu tawa wa wilaya ya Singida (DAS) Wilson Shimo. |
|
Mwakilishi wa mgeni rasimi katibu tawa wilaya ya Singida Bw Wilson Shimo akifungua hafla hiyo. |
|
Mkurugenzi wa ESTL Bw Joshua Ntandu akielezea kazi za shirika hilo . |
|
INSP Iddah John -Mratibu dawati la jinsia na watoto wa jeshi la polisi mkoa wa Singida akifafanua namna wanavyotatua matatizo mbalimbali na chanagamoto zake. |
|
Mh Mussa Sima amelishairi shirika hilo kujaribu kukutana na kamati ya bunge usika na mambo ya kijamii ili kupata fulsa ya kujadiliwa katika vikao vya bunge. |
|
Bi Severina Kilala ni afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Singida akichangia mada. |
|
Bw Victor Exavery Kavusha Afisa Tarafa Unyakumi nae akichangia mada juu ya maswala ya wazazi wa kike kuhusika moja kwa moja na ukeketaji |
|
Mratibu wa ubora wa huduma za afya wilaya ya Singida (DQIFP) Dr Getrude Mughamba akifafanua namna wanavyoto elimu kwa kina mama pindi wanapofika klinik. |
Mkoa wa
Singida umetajwa kuwa
miongoni mwa mikoa
inayoongoza kwa vitende
vya ukeketaji kwa
wanawake.
Katika kikao
cha uzinduzi wa
mradi awamu ya
pili katika halmashauri ya
manispaa ya Singida
wa kutokomeza ukatili
wa kijinsia mradi
unaoendeshwa na shirika
la ESTL unatarajia
kuzifikia kata [15]hadi
kufikia ukomo wake ambaye
ni miaka miwili.
Aidha akizindua
mradi huo mkuu wa
mkoa wa SINGIDA
ambaye amewakilishwa na
katibu tawala wilaya
ya SINGIDA WILSON SHIMO ametoa
rai kwa viongozi wote
wanaolengwa na mradi
huo kutoa ushirikiano kwa
shirika hilo ili kuhakikisha
mradi unafanikiwa kwa
kuondoa vitendo vya
ukeketaji.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa
bodi ya shirika
hilo ambaye ni mkuu
wa mkoa wa KILIMANJARO
MAMA ANNA MGHWIRA
amesema shirika limejielekeza
katika mipango mikuu
minne katika kutimiza
wajibu wake wa
kutatua changamoto za
maendeleo zinazozikabili
jamii mkoa wa
SINGIDA na maeneo
mengine nchini.
Shirika la [ESTL]
yaani EMPOWER SOCIETY TRANSFORM
LIVE,limekwisha tekeleza mradi
wake awamu ya
kwanza katika kata nne
za halmashauri ya
SINGIDA na leo
limezindua mradi awamu
ya pili katika
kata za UNYAMIKUMBI,UNYIANGA pamoja
na MTAMAA zilizopo
katika halmashauri ya
manispaa ya SINGIDA.
Tuandikie Maoni Yako Hapa
0 Comments