Theresa May amesema ataunda serikali
iliyo na uhakika wa siku za usoni, akiungwa mkono na chama cha DUP
Akizungumza baada ya kutembelea ikulu ya Buckingham, alisema ni
chama chake tu kilicho na "uhalali" wa kutawala, licha ya kushindwa
kupata wingi wa wabunge katika uchaguzi wa Alhamisi.
Alisema angeweza kujiunga na "rafiki" zake wa DUP na
"kufanya kazi" inayohusiana na Brexit.
Lakini wanachama wa Leba walisema wao ndio "washindi
halisi" huku wanademokrasia huria wakisema Bi May unapaswa kuwa na
"aibu" ya kuendelea na kazi.
Katika kauli fupi nje ya barabara ya Downing, iliyofuatwa na
mkutano wa dakika 25 na Malkia, Bi May alisema ana nia ya kuunda serikali
ambayo inaweza "kutoa uhakika na kuipeleka Uingereza mbele kwa wakati huu
muhimu kwa nchi".
Akizungumzia "uhusiano imara" aliokuwa nao na DUP
lakini akitoa maelezo kidogo ya jinsi mpangilio wao unaweza kufanya kazi,
alisema serikali itaweza "kuongoza nchi katika mazungumzo muhimu ya
Brexit" yanayofaa kuanza katika muda wa siku 10 tu.
"Vyama vyetu viwili vimekuwa na uhusiano bora kwa miaka
mingi," alisema.
"Na hii inanipa mimi imani ya kwamba tutaweza kufanya kazi
pamoja kuboresha maslahi ya Uingereza."
Kiongozi wa DUP Arlene Foster alithibitisha kwamba amezungumza
naye Bi May na kuwa watawasiliana zaidi ili "kujadili jinsi wataweza
kuleta utulivu kwa taifa, wakati huu wa changamoto kubwa".
Licha ya kuwa wanafanya bidii siku zote kwa ajili ya
"mpango bora" kwa Ireland ya Kaskazini na watu wake, alisema chama
chake daima kinataka manufaa yaliyo bora kwa Uingereza kwa jumla.
Baada ya matokeo ya maeneo mengi kutangazwa, Theresa May
alipungukiwa na wabunge 12 ukilinganisha na wabunge aliokuwa nao wakati wa
kuitisha uchaguzi huo.
Kiongozi wa chama cha Leba Jeremy Corbyn amesema pia kwamba yuko
"tayari kutumikia".
0 Comments