Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi amesema
angependa kusalia na klabu yake kwa siku zilizosalia katika taaluma yake.
''Ni
kitu ambacho nimekuwa nikikitazamia na ni kitu nilichokuwa nikikitaka,"
alisema.
Kiungo
huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na Barcelona akiwa na umri
wa miaka 13, akashiriki mechi yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 17 na
amefunga zaidi ya magoli 500 akiwa na klabu hiyo.
Messi
ameshinda taji La liga mara nane, Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara nne na tuzo
mchezaji bora duniani Ballon d'Or mara tano.
Msimu
uliopita chini ya kocha Luis Enrique, Barcelona walikuwa katika nafasi ya pili
kwa ligi ya La Liga, alama tatu chini ya mabingwa watetezi wa Ligi ya Klabu
Bingwa Ulaya Real Madrid.
Walishindwa
3-0 katika robo fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Juventus.
Enrique
alitangaza mwezi Machi, kwamba angeiaga klabu hiyo baada ya mkataba wake wa
miaka mitatu kumalizika, mechi yake ya mwisho ilikuwa ni pale Barca
walipojinyakulia kombe la Copa Del Rey .
Messi
alifunga bao la ufunguzi walipoichapa Alaves mabao 3-0 na kupata ushindi.
Messi
ambaye alikuwa wa pili nyuma ya mshambuliaji wa Real, Cristiano Ronaldo katika
tuzo ya Ballon d'Or, aliuambia mtandao wa Barcelona lengo lake ni ''kujaribu
kuimarika kila msimu hadi mwisho, na hilo ndilo lengo langu la msimu ujao.''
0 Comments