GWIJI wa Brazil, Pele amesema ni kichekesho
kumuita mshambuliaji wa Juventus na Argentina, Paulo Dybala ni Diego Maradona
mpya.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa
sasa ni mmoja wacheza gumzo kubwa Ulaya wenye umri mdogo baada ya kujiunga na
Kibibi Kizee cha Turin kutoka Palermo mwaka 201
Paulo Dybala |
Dybala amefunga mabao 30 kwa misimu yake
miwili ya kucheza Serie A, akishinda mataji katika misimu yote pamoja na
kuisaidia timu hiyo kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Pamoja na hayo, vigogo hao wa Italia
walisambaratishwa na Real Madrid mjini Cardiff kwa kufungwa 4-1 huku mashabiki
wakimponda kinda huyo baada ya kucheza ovyo.
Na akatawala kwenye midomo ya watu baada ya
kucheza ovyo pia jana licha ya Argentina kushinda 1-0 dhidi ya Brazil.
"Si mzuri kama watu
wanavyosema,"amesema mshindi huyo wa Kombe la Dunia mara tatu.
"Wanasema atakuwa Maradona mwingine,
lakini kitu pekee anachofanana na naye ni kutumia mguu wa kushoto
tu,"amesema Pele.
0 Comments