MRADI WA REA AWAMU YA 3 WAZINDULIWA MKOANI SINGIDA


Waziri wa nishati Prof Muhongo na kulia ni  balozi wa Norway Amb Hamme- Hanie Kaarstad na kushoto balozi wa Sweden Amb Katarina Rangnitly wakizindua mradi huo  wilayani Manyoni Singida.





Afisa habari kwa umma wa Tanesco mkoa wa Singida Whitiy akionyesha kifaa cha kuungia umeme cha bei nafuu.

Waziri wa Nishati na Madini,Prof.Sospeter Muhongo amesema zaidi ya vijiji 7,000 kati ya vijiji 12,000 vilivyopo nchini vinatarajia kunufaika na umeme utakaosambazwa na wakala wa usambazaji nishati ya umeme vijijini (REA) awamu ya tatu ifikapo mwaka 2019.
Prof.Muhongo amesema hayo kwenye uzinduzi wa mradi wa kusambaza umeme vijiji awamu ya tatu katika Mkoa wa Singida,uliofanyika katika Kijiji cha Mkwese,wilayani Manyoni.
Hata hivyo Waziri Muhongo amesema  ili miradi hiyo iweze kukamilika kunahitaji fedha zinazotokana na vyanzo viwili vya fedha vinavyotegemewa kufanikisha shughuli hiyo ya miradi.
Kwa mujibu wa Prof.Muhongo vyanzo hivyo ni pamoja na asilimia 50 kutoka katika vyanzo vya ndani na asilimia nyingine 50 inatokana na misaada kutoka nchi wahisani wakiwemo walipa kodi wa Norway na Sweden. 

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments