Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dr. Anna Peter Makakala
amefanya mabadiliko makubwa ya Viongozi wa Uhamiaji wa Mikoa mbalimbali hapa
nchini pamoja na kuwateua Wakuu Wapya wa mikoa kushika nyadhifa hizo katika
Mikoa iliyopo Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.
Katika Mabadiliko haya Naibu Kamishna wa Uhamiaji Sixstus
Faustine Nyaki aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza amehamishiwa
mkoa wa Simiyu wakati aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Rukwa Naibu
Kamishna wa Uhamiaji Selemani Bandiho Kameya amehamishiwa
Mkoa wa Tabora.
Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, Naibu Kamishna wa Uhamiaji
Asumsio Paulus Achacha amehamishiwa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mkuu wa
Uhamiaji Mkoa wa Manyara Naibu Kamishna Peter Jerome Kundy
amehamishiwa Mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi
Ali Mohamed ambaye amehamishiwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji mkoa wa
Arusha.
Naibu Kamishna wa Uhamiaji Mkemi Mhina Seif
ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja, Naibu Kamishna wa
Uhamiaji Muhsin Abdallah Muhsin ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa
Kaskazini Unguja, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Said Omary Hamdani
ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharibi na Naibu
Kamishna wa Uhamiaji Othman Khamis Salum ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji
Mjini Magharibi Unguja.
Katika mabadiliko hayo baadhi ya Wakuu wa Uhamiaji wa Mikoa
wamebaki katika Vituo vyao vya kazi vya awali akiwemo aliyekuwa Mkuu wa
Uhamiaji Mkoa wa Morogoro Naibu Kamishna wa Uhamiaji Safina Muhindi, Mkuu
wa Uhamiaji Mkoa wa Lindi Naibu Kamishna wa Uhamiaji George Kombe, Mkuu wa
Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Naibu Kamishna wa Uhamiaji Hilgaty Laurent
Shauri, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Singida Naibu Kamishna wa Uhamiaji Faith
Alexander Ihano na Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mara Naibu Kamishna
Fredrick Eustace Kiondo.
Wengine waliobaki kwenye vituo vyao vya awali ni pamoja
na Naibu Kamishna wa Uhamiaji Abdallah Ramadhani Towo
mkoa wa Kagera na Naibu Kamishna wa Uhamiaji Anastazia Gasper
Ngatunga mkoa wa Shinyanga.
Katika mabadiliko hayo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr.
Makakala pia amewateua Viongozi wa Uhamiaji wa Mikoa wapya katika baadhi
ya mikoa hapa nchini ambapo Naibu Kamishna wa Uhamiaji Mary Francis
Palmer kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Naibu
Kamishna wa Uhamiaji Plasid Mazengo, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa
wa Pwani, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji James Andrew Mwanjotile,
Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi Hope Jaffer Kawawa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa
Iringa, na Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Hosea Alphonce
Kagimbo Mkoa wa Njombe.
Wengine ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji Rashid Salum
Magetta Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Songwe, Naibu Kamishna wa
Uhamiaji Carlos John Haule, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Rukwa, Naibu
Kamishna wa Uhamiaji Julieth Deodatus Sagamiko Mkuu wa Uhamiaji Mkoa
wa Manyara, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Albert Joseph
Rwelamila, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro na Naibu Kamishna
wa Uhamiaji Paul Laurent Eranga, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa
Mwanza.
Naibu Kamishna wa Uhamiaji Crispin Crispin Ngonyani ameteuliwa
kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa
Uhamiaji Shaban Omar Hatibu Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa
Katavi, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Remigius Ibrahimu
Pesambili Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kigoma na Mrakibu Mwandamizi wa
Uhamiaji Novaita Edmund Mrosso ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa
Mbeya.
Aidha Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Bakari Mohamed Ameir
ameteuliwa kuwa Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Abeid Amani Karume [AAKIA] na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji
Fulgence Andrew Mutarasha kuwa Mkuu wa Uhamiaji Kituo cha Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere[JNIA].
Imetolewa na
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini
Dr. A. P. Makakala
0 Comments