soko la kimataifa la vitunguu Misuna Singida |
Mkuu wa wilaya ya Singida Bw Elias Tarimo wakati akiongea na wakulima na wafanyabiashara.
|
MKUU wa Wilaya ya
Singida amepiga marufuku wafanyabiashara wa vitunguu kutoka nchi jirani za
Kenya,Uganda,Ruanda,Burundi,Zambia, Kongo na Malawi kwenda kununu vitunguu
kweneye mashamba ya wakulima vijijini na badala yake amewataka kwenda kununua
kwenye soko la kimataifa la vitunguu,lililopo Manispaa ya Singida.
Tangazo hilo la zuio
lilitolewa na Mkuu wa wilaya ya Singida,Bwana Eliasi Tarimo baada ya kupokea
malalamiko ya wafanyabiashara kutoka soko la kimataifa la vitunguu, kulalamikia
kuwa wafanyabiashara wanaotoka nchi hizo kuwa wanakwenda kununua vitunguu kwenye
mashamba ya vijijini na hivyo kusababisha biashara katika soko hilo kudorora
huku serikali ikikosa mapato yake.
Hata hivyo Bwana
Tarimo hakusita kuwaeleza umuhimu wa tangazo hilo kuwa ni kuhakikisha
mkulima,mfanyabiashara wa kati na mfanyabaishara mkubwa kila mmoja ananufaika
na shughuli yake anayoifanya na kuwataka baada ya kufanyabiashara zao wasisite
kwenda kulipa kodi ili serikali iweze kuwaletea maendeleo kwenye maeneo yao.
Nao baadhi ya
wafanyabiashara wa vitunguu katika soko hilo la kimataifa,Bwana Jonathani
Mpinga amesema kuwa serikali haina budi kuweka usawa wa sheria ya kuzuia
ujazaji kwa njia ya lumbesa kwa mikoa yote badala ya sheria hiyo kutumika
katika Mkoa wa Singida peke yake.
Ameweka bayana kwamba
akiwa mfanyabiashara wa zao hilo amekwenda katika masoko ya Moshi na Mang’ola
hajawahi kuona sheria ya kukataza ujazo wa lumbesa kama inavyokatazwa katika
Mkoa wa Singida na hivyo kuishauri serikali kuwa na kauli moja kwa nchi nzima
ili wanunuzi wasije wakawakimbia katika soko hilo.
0 Comments