Vyama vya kisiasa nchini Algeria
vimeridhia kuweka picha za wagombea wa kike kwenye mabango yake.
Vyama vingi vimekua vikiweka picha za mitandio bila kuwepo na
uso wa mgombea.
Hata hivyo picha za wagombea wa kiume zimetawala kwenye mabango.
Maafisa wa uchaguzi wameagiza vyama kuanza kuweka picha za
wagombea wa kike la sivyo vitaondolewa kwenye usajili.
Hatua hii imevutia hisia tofauti kutoka kwa wagombea wa kika na
kiume.
Mmoja wa wagombea Fatma Tirbakh wa chama cha 'National Front For
Justice' amesema eneo anakotoka kuna mila na itikadi kali dhidi ya wanawake
kujionyesha hadharani.
Hata hivyo amesema anataka picha yake kuwekwa kwa bango, kinyume
na awali ambapo ni jina tu lililowekwa.
Chini ya sheria ya mwaka 2012, nchini Algeria, vyama vya kisiasa
vinatakiwa kuwateuwa kati ya asili mia 20 na 50 ya wanawake kama wagombea.
Algeria siyo taifa pekee ambapo wagombea wa kike hawaweki picha
zao kwenye mabango wakati wa kampeini.
Nchini Misri vyama vyenye itikadi kali za kidini vilitumia picha
ya maua badala ya picha za wagombea wa kike kwenye uchaguzi wa ubunge wa mwaka
2011 na 2012.
0 Comments