MABINGWA wa Ligi Kuu ya Azam Uganda,
KCCA wameweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza nchini humo kufuzu hatua ya
makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika Jumamosi.
Hiyo inafuatia kuitoa Al Masry ya Misri kwa penalti 4-3 mjini Cairo baadaya sare ya kumla ya 1-1 kufuatia kila timu kushinda 1-0 nyumbani.
KCCA Jumamosi imefungwa hii imefungwa 1-0 ikitoka kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Phillip Omondi bao pekee la Derrick Nsibambi.
Kipa Benjamin Ochan leo ameokoa michomo miwili ya
penalti na kufunga moja sawa na Geofrey Sserunkuma, Muzamiru Mutyaba na Timothy
Dennis Awany kuipa ushindi huo KCCA.
KCCA
iliangukia kwenye mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la
Shirikisho baada ya kutolewa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwenye Ligi
ya Mabingwa.
0 Comments