Mkuu wa wilaya ya Ikungi na kaimu mkuu wa wilaya ya Singida Mh Miraji Mtaturu akizungumza na madiwani wa manispaa ya katika kikao cha baraza la bajeti.
|
KAIMU mkuu wa wilaya ya Singida,Miraji Mtaturu,ameagiza mkakati
wa kutoa huduma ya chakula katika shule za msingi na sekondari,utekelezwe kwa
kasi kubwa,ili pamoja na mambo mengine,taaluma iweze kupanda.
Mtaturu ambaye ni mkuu wa wilaya ya Ikungi,ametoa agizo hilo
jana (1/3/2017) wakati akizungumza mbele ya kikao cha kawaida baraza la
madiwani, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa manispaa hiyo.
Akisisitiza,alisema halmashauri ya manispaa ya Singida,ikitaka
ufaulu uongezeke ni lazima huduma ya chakula cha mchana, ikapatikane katika
shule zake.
“Wapo baadhi ya wanafunzi wanatembea kilometa tano kwenda
shuleni,na mbaya zaidi anatoka nyumbani hata bila kunywa uji.Huyu kuna
uwezekano mkubwa akalala uzingizi darasani.Lakini kama kuna huduma ya
chakula,hilo halitatokea”,alisema kaimu DC huyo.
Aidha,Mtaturu amezitaka kamati za shule ziwajibike kwa suala la
chakula,sambamba na kuhakikisha miundo mbinu inaboreshwa.
Katika hatua nyingine,amewakumbusha madiwani wajibu wao wa
kusimamia mapato na matumzi ya mapato ya halmashauri.
Akisisitiza,alisema mashine EFD za kutolea stakabadhi/risiti ni
lazima zitumiwe na wakusanya mapato,ili kuondoa uwezekano wa udokozi wa mapato.
“Kwenye vyanzo vya mapato,wekeni makadrio ili yasipofikiwa,mpate
uwezo wa kuhuji ni kwa nini hayajafikiwa.Hatua hiyo itasaidia kuthibiti
wadokozi kujinufaisha binafsi”,alisema.
Aidha,kaimu mkuu huyo wa wilaya,amewaomba madiwani kuanzisha
dawati la mapokezi ya kero za wananchi,ili yaweze kushughukiwa mapema kabla
hayajaleta athari kubwa.
Wakati huo huo,Mtaturu amewaomba wakahimize wakulima kutumia
mvua hizi zinazoendelea kunyesha,kulima mazao yanayokomaa mapema.
Pia amewataka wahakikishe kila kaya inapanda miti kumi,
ili siku ikifika halmashauri ya manispa Singida,iwe ya kijani wakati wote.
Diwani wa kata ya Kisaki Mozesy Ikaku akitoa shukrani kwa niaba ya madiwa baada ya mkuu wa wilaya kuzungumza na madiwani hao.
|
madiwani sambamba na mbunge wa jimbo la Singida Mjini Mh Mussa Sima wenye shati la blue wakimsikilza mkuu wa wilaya.
|
0 Comments