Keki maalumu yenyeujumbe |
Waziri wa afya ,maendelea ya jamii,jinsia ,wazee na watoto Ummy Mwalimu akiongea katika kongamano hilo.
|
keki ikikatwa kuashiria umoja na upendo kwa viongozi kinamama wa Singida. |
kulia ni Dr Nchimbi mkuu wa mkoa wa Singida na waziri Ummy mwalimu. |
kinamama wakimsikiliza waziri katika ukumbi wa FDC |
NA
JENESTA ZEDEKIA
Imeelezwa
kuwa ukombozi wa kweli kwa mwanamke ni elimu hivyo jamii imetakiwa kupinga
ukatili dhidi ya watoto wa kike kwani ndio Taifa la kesho.
Ameyasema
hayo waziri wa afya,maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu
katika kongamano la wanawake lililofanyika katika ukumbi wa FDC mkoani Singida
likiongozwa na mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Rehema Nchimbi.
Ummy
amesema akiwa ndiye mwenye dhamana ya elimu na afya amewataka wanawake kuwa
mstari wa mbele katika kuhakikisha watoto wa kike wanapata elimu.
Amesema
ili kufikia Tanzania ya viwanda lazima jamii iweze kuwa mstari wa mbele katika
kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
Waziri
wa afya,maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu yupo mkoani
hapa akitarajia kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
ambayo uadhimishwa March,8,kila mwaka.
0 Comments