Kamada wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimga akielezea juu ya fisi watatu.
|
Wanahabari wakiwakazini mkoani Singida. |
DK Ng"hungu kuzenza akitoaufafanuzi |
FISI watatu wamejeruhi
vibaya watu wanane katika sehemu mbali mbali za miili yao na kulazwa katika
Hospitali ya Mkoa wa Singida,Hospitali ya wilaya ya Iramba na Hospitali ya
Misheni Haydomu,wilayani Mbulu,Mkoani Manyara.
KAMANDA wa polisi Mkoa
wa Singida,ACP.DEBORA MAGILIGIMBA amesema tukio hilo limetokea Feb,14 hadi
Feb,16,mwaka huu na kwamba kati yao watatau wana hali mbaya na watano hali zao
zinaendelea vizuri.
KWA upande wake Kaimu
Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida,DK.NG’HUNGU KUZENZA
amekiri kumpokea mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Mtisi,Manispaa
ya Singida aliyetambulika kwa jina la FARIDA RAMADHANI(9) na kwamba kumekuwepo
pia mbwa wanaodhaniwa kuwa na kichaa ambao nao wamekuwa wakiwauma wananchi
katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Singida.
KUFUATIA tukio la watu
kuumwa na fisi Kamanda wa polisi Mkoa wa Singida anatumia fursa hiyo kutoa wito
kwa wananchi wa Mkoani humo wanapoona wanyama ambao siyo wa kufugwa watoe
taarifa kwa viongozi wao wa ngazi zote ili waweze kuchukua hatua za haraka na
kuwanusuru wananchi wao.
0 Comments