MIPANGO YA MUZIKI YA PRODUZA MAN WALTER NDANI YA MWAKA HUU NDIYO HII HAPAAA……


Old Combination Sound
New Combination Sounds Studio
Producer Man Walter kutoka studio za Combination Sounds ameweka wazi mipango yake ya muziki ndani ya mwaka huu.

Mkali amesema amaejipanga ndani ya mwaka huu kuwasaidia wasanii wanaochipukia katika muziki pamoja na kuwarejesha kwa mara nyingine tena wasanii waliopotea katika gemu ambao walifanya vizuri hapo zamani.

Man Maji amefunguka hayo wakati akipiga story na kipindi cha Standard Mix cha Standard Radio Alhamis hii mkali alisema…
“Kwanza kuja na kazi mpya kutoka kwa wasnii wachanga lakini pia bado ni uleule mwendelezo  kuwasaka wale wasanii ambao walipotea kwenye g ame nakujaribu kujaribu kufanya harakati za kuwarudisha kiwemo pia ile mikakati tunaiendeleza yaakumrudisha 20 percent”alisema mkali Walter

Produza huyo pia amesema kuna kazi ambayo amepanga kufanya na Band ya Twanga Pepeta hivi karibuni.
“natarajia pia  kufanya kazi na Twanga Pepete najaribu kuwaweke ladha za kisasa hivi pia kuchanganya na muziki wa bendi na muziki mingi pia’’aliongeza mkali


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments