Imeelezwa kuwa matumizi yasiyo sahihi ya
barabara yanaweza kupunguza nguvu kazi na kusababisha vilema pamoja na
majeruhi ya kudumu kwa watumiaji wa vyombo vya moto na waliowabeba.
Hayo yamesemwa na Bw.Paul David amabye ni mtunza nidhamu
wa polisi wa wilaya ya Singida wakati akizungumza na kipindi cha ZINDUKA cha STANDARD RADIO mjini SINGIDA ambapo
amewataka waendesha vyombo vya moto kama vile pikipiki na bajaji kuwa makini
katika uendeshaji wao.
Aidha amewataka waendesha pikipiki kuhakikisha wanavaa kofia
ngumu ikiwa ni pamoja na kufunga mikanda ya kofia hiyo ili kuweza kujikinga na
ajali pale inapotokea.
Hata hivyo amemalizia kwa kusema kuwa pale wananchi wasipo
ridhika na huduma inayotolewa na maafisa usalama barabarani waweze kutoa
taarifa kwa vyombo vya sheria.
0 Comments