Afisa utawi wa jamiii hospitali ya mkoa Singida Magret Henjewele |
Wito
umetolewa kwa kina mama wote ambao wanafanyiwa ukatili wa kijinsia na waume zao
kutoa ushirikiano kwa vyombo vya sheria ili sheria iweze kuwabana watuhumiwa na
hao lengo likiwa ni kukomesha vitendo vya unyanyasaji kwa kina mama.
Akizungumza
na Standard radio ofisini kwake afisa ustawi wa jamii katika hospitali ya mkoa
wa Singida Bi. Magreti Henjewele amesema wamekuwa wakiwapokea wagonjwa wengi hususani
wanawake ambao wamepigwa na kuumizwa na waume zao lakini baada ya kupona huwa
wanaamua kusamehe na kuwaficha wahalifu hao.
Amesema
chanzo kikubwa kinachopelekea ugomvi hadi mama kuumizwa ni maswala ya kiuchumi
ambapo kina baba wengi wamekua tegemezi katika familia zao kwa kuwasubiri kina
mama wakatafute na wao kuja kulazimisha kutumia pesa hizo kwa maslahi yao
binafsi.
Bi.
Henjewele amesema wamekuwa wakiwapokea wagonjwa wa namna hiyo hadi kumi huku
wengi wao wakiwa na hali mbaya na wengine kupoteza maisha wakati wakipatiwa
matibabu.
0 Comments