Millard Ayo,Ankal Issa Michuzi,Abdallah Mrisho na Askofu wa Ayo TV |
Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitaka Michuzi TV,
AYO TV na
Global TV kusitisha huduma zao za TV mtandaoni hadi hapo kanuni za usajili
rasmi ambazo mamlaka hiyo imesema inaandaa kwa
huduma hizo
zitapokuwa tayari.
Barua hiyo,
iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu Mhandisi James
Kilaba
tarehe 30 January mwaka huu, imevitaka vyombo hivyo ambavyo vinapendwa
sana nchini
na nje ya nchi kuacha mara moja kutoa huduma za TV mtandaoni.
"Kwa
mujibu wa section 13 (1) of the electronic and
postal
communications Act Cap 306, sheria za Tanzania zinahitaji watoa huduma
zozote za
aina hiyo wanahitaji leseni kutoka mamlaka ya mawasiliano",
imesema
barua hiyo.
Wamiliki wa
mitandao hiyo - Millard Ayo, Ankal Issa Michuzi
na Abdallah
Mrisho - wameeleza
kushtushwa
kwao kwa agizo hilo la ghafla, tena wakati hata kanuni zenyewe
hazijawekwa.
"Gloval
TV ipo
tayari hata leo kukamilisha taratibu za usajili - kama zingekuwepo - na
kwa sababu
bado kukamilika tunaomba kupewa muda zaidi wa kuendelea kutoa huduma hii
ya bure tukiwa chini ya uangalizi wakati
tunasubiria
kanuni hizo mpya," alisema Abdallah Mrisho, Meneja Mkuu wa
Global
Publishers.
Ankal
Michuzi na Millard Ayo waliunga mkono kauli hiyo na kwa pamoja
watatu hao
wameomba kuonana na mkurugenzi wa TCRA ili kuwasilisha maombi rasmi
ya
kuruhisiwa kuendelea kutoa huduma hiyo kwa muda wakati kanuni
zikisubiriwa.
Bahati
mbaya Mhandisi Kilaba alikuwa safari na swala hilo limepangwa
kushughuliwa
ataporejea wiki ijayo.
"Ukizingatia
kwamba tumekuwa tunatoa huduma hii kwa muda mrefu na haijulikani kanuni
zitakuwa tayari lini tunaomba TCRA iangalie namna ya kufanya ili wananchi
wanaotutegemea sana kwa taarifa mbalimbali wasikose huduma hii", alisema
Ankal. Hata hivyo vituo hivyo vitatu vinaendelea kuhudumu nje ya mwenendo
wa TV mtandao, ambapo kwa sasa vitaendelea kuhudumu kwa kutumia majina ya
blog zao.
Na Sultani Kipingo, Globu ya Jamii
0 Comments