Mrakibu msaidizi na kamanda wa zima moto na uokoaji mkoa wa Singida Hamis Lutengo. |
Magri ya jeshi ya zimamoto mkoani Singida ambayao hayafanyi kazi tokea mwaka uliyopita mpaka sasa yakisubili fedha za ukarabati. |
Jeshi la zima moto mkoani Singida limeahidi wilaya zote za mkoa wa
Singida kuwa na vituo vya zima moto ili kuhakikisha usalaama wa raia pamoja na
mali zao
Mrakibu msaidizi na kamanda wa zima moto na uokoaji mkoa wa Singida
Hamis Lutengo ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake
Aidha Bw.Lutengo amesema kila mwananchi ana wajibu wa kuzima moto
pale unapotokea ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa jeshi la zima moto ili
kupata msaada zaidi
Kwa upande mwingine Bw Lutengo amezungumzia malalamiko ya wananchi kuhusu
vyeti walivyoahidiwa kwa muda mrefu.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Singida mjini Musa Ramadhan
Siima amesema kuwa hoja hiyo ilitolewa kwenye baraza la madiwani ambapo baada
ya hoja hiyo kujadiliwa elimu ilitolewa ili kuondoa mgogoro huo baina ya
wafanyabiashara na kikosi cha zima moto mkoa.
0 Comments