AZAM FC YATIMUA BENCHI LAKE LA UFUNDI

Zeben Hernandez (kulia)akiwa na msaiziwake  
Kalimangonga ongala
AZAM FC imetimua Benchi la Ufindi chini ya kocha wao Zeben Hernandez kwa kile kilichodaiwa kuwa ni mwenendo mbovu wa timu hiyo tajiri kwenye Ligi Kuu ya Vodacom.

Azam imekuwa ikipata matokeo mabaya ambayo yamepelekea kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi huku matumaini ya kuwania ubingwa ama nafasi ya pili yakiwa yamefifia kabisa.

Habari kutoka ndani ya Azam zimesema kuwa tangu jana Jumanne uongozi wa klabu hiyo ulikuwa na mazungumzo na makocha hao ambapo leo wamefikia makubaliano ya kuvunja mikataba yao.

Inadaiwa kuwa kumetokea na sintofahamu kati ya wamiliki wa timu hiyo hasa upande wa usajili kwa kuwaacha nyota wao bila sababu za msingi akiwemo Jean Mugiraneza ambapo awali ilielezwa kuwa kocha huyo Mhispania alidai kutokuwa na matumizi naye hivyo aachwe.


Chanzo kutoka ndani ya Azam FC kinasema kuwa kocha wa Majimaji, Kally Ongalla ndiye anayetajwa kuja kushika mikoba hiyo. Kally aliwahi kuifundisha Azam akiwa kocha msaidizi chini ya Stewart Hall pamoja na Josepg Omog.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments