Rais Barack Obama wa
Marekani amewasili nchini Ugiriki leo ikiwa ni kituo chake cha kwanza katika
ziara yake ya mwisho akiwa rais wa Marekani.Katika hotuba yake ya kwanza tangu
kufanyika kwa uchaguzi wa Marekani, rais Barack Obama ameelezea hali ya kujiamini
kwamba Donald Trump atataka kuendeleza mkakati wa Marekani wa washirika.
Rais Obama aliongeza
kwamba kikosi chake kitaongeza kasi ya juhudi za kuhakikisha makabidhiano
yasiyokuwa na matatizo kwa utawala wa Trump, baada ya kuelezea wasi wasi hapo
kabla kwamba Trump hafai kuwa rais wa nchi hiyo.
Rais Obama pia alitaka
kuwahakikishia viongozi wa dunia baada ya kampeni ya uchaguzi ya rais mteule
Trump ambayo imesababisha taifa hilo kugawika , na kutawaliwa na madai ya
ubaguzi , udhalilishaji wa wanawake, na chuki dhidi ya wageni.
Trump pia ametoa
matamshi ya maridhiano kuhusiana na wanawake na makundi ya jamii ya wachache
baada ya uchaguzi. Kabla ya kuanza ziara yake ya mwisho akiwa rais wa Marekani
ambayo pia itamfikisha Ujerumani, Obama pia alisifu uhusiano mzuri wa kikazi na
kansela wa Ujerumani Angela Merkel, ambaye amemweleza kuwa huenda ni mshirika
wake wa karibu zaidi kimataifa.
0 Comments