Waziri mkuu nchini Jamhuri ya
Demokrasi ya Congo Augustin Matata Ponyo, amejiuzulu na kutoa fursa ya
kuteuliwa mrithi wake kuongoza serikali ya mpito.
Kujiuzulu kwa bwana Ponyo ni sehemu ya makubaliano yaliyotiwa
sahihi mwezi uliopita kati ya serikali ya Rais Joseph Kabila na baadhi ya vyama
vya upinzani ya kuhairisha uchaguzi wa urais hadi mwezi Aprili mwaka 2018.
Wapiga kura nchini DRC walistahii kupiga kura mwezi huu
kumchagua mrithi wa Rais Kabila, wakati wa kumalizika kwa muhula wake wa
mwisho.
Vyama vikuu vya upinzani vinakataa kuhairishwa kwa uchaguzi
vikisema kuwa hiyo ni njama ya Rais Kabila ya kusalia madarakani.
Baraza lote la mawaziri lilijiuzulu pamoja na bwana Ponyo.
0 Comments