Singida
–
Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amekabidhi magari mapya kwa wakuu wa wilaya
za Iramba, Ikungi, Manyoni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Singida, ikiwa
ni hatua ya kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.
Makabidhiano
hayo yalifanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, ambapo
Dendego aliwataka wakuu hao wa wilaya kuyatunza magari hayo ili yadumu na
kusaidia katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
“Nawasihi
myatumie magari haya kwa matumizi yaliyokusudiwa na myatunze ili yaweze kudumu
kwa muda mrefu na kuwasaidia kutekeleza majukumu yenu kikamilifu,” alisema RC
Dendego.
Awali,
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Fatuma Mganga, akimkaribisha Mkuu wa
Mkoa, alisema hadi sasa mkoa huo umepokea magari yenye thamani ya zaidi ya
shilingi bilioni mbili, yakiwemo magari ya huduma za afya na shughuli nyingine
za utawala.
“Kupitia
jitihada za Serikali, Mkoa wa Singida umepokea magari ya thamani ya zaidi ya
shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma mbalimbali,
ikiwemo sekta ya afya,” alieleza Dkt. Mganga.
Makabidhiano
hayo ni sehemu ya mpango wa Serikali wa kuimarisha miundombinu ya kiutendaji
katika ngazi ya wilaya na kuhakikisha wananchi wanahudumiwa kwa ukaribu na kwa
wakati.
0 Comments