NA MWANDISHI WETU
MFANYABIASHARA mstaafu mkazi wa Singida mjini,Hamisi Ng’eni
(61),amefariki dunia baada ya nyumba yake kuteketea kwa moto, ambayo hadi sasa
chanzo chake hakijajulikana.
Mwenyekiti wa mtaa wa Unyakae manispaa ya Singida,Abbakari
Athumani Kimu,amesema moto huo ulioanza kuonekana saa tatu usiku juni mbili
mwaka huu.Uliendelea hadi ukateketeza karibu mali zote.
Akifafanua alisema “kwa kawaida marehemu baada ya kufiwa na mke
wake miaka miwili iliyopita,amekuwa na utamaduni wa kulalal peke yake kwenye
nyumba hiyo kubwa”,alisema na kuongezeka;
“Kutokana na utamaduni huo,majirani walikuja kutambua moto huo,
baada ya nyumba karibu yote kushika moto”.
Alisema mwenye nyumba huyo ambaye ametolewa kwenye chumba chake
cha kulala na mwanajeshi ambaye jina lake halijafahamika,hakuwa na miguu wale
mikono.Yote imetekekea kwa moto.
Pia amesema wakati zoezi la kuzima
moto linamalizika,vyombo na mali zingine mbalimbali iliyokuwa katika
vyumba vyote,ilikuwa imeteketa.
Jirani yake na marehemu Ng’eni,Amita Ramadhani
Idd,alisema akiwa wa kwanza kufika kwenye tukio hilo,aliokota simu ya
Nge’ni ikiwa imetupwa nje jirani na dirisha la mwenye mali.
Alisema kuwa Nge’ni baada ya kufiwa na mke wake, alianza kuugua mara kwa mara.
Katika hatua nyingine, alisema kwa sasa manispaa ya
Singida,inatakiwa kuweka mikakati thabiti kuhakikisha inakuwa na vyombo vya
zima moto ikiwemo maji ya kukidhi mahitati ya sasa, na wakati ujao.
“Kwa kweli huduma ya maji ya kuzimia moto,kwa sasa ipo duni
kupindukia.Jana zimamoto ilipo fika hapa,ilikuwa na maji machache
sana.Haikuchukua dakika,yalikwisha.Tukaanza kuhangaika huku na huko na sehemu
nyingi zinazotumika kutunza maji hayo,hazikuwa na maji”,alisema kwa masikitiko.
Hata hivyo,Amita alitumia fursa hiyo kuishukru kampuni ya Maount
Meru,kwa msaada wake wa kutoa msaada wa bure wa maji,na pia gari la kumbembea
maji..
Kuhusu mazishi,mwenyekiti Kimu alitangaza kuwa yanatarajiwa
kufanyika jana (03/06/2024) na ni wapi atazikwa,itatangazwa
watakapofika watoto wake Ng'eni kutoka jijni Dar-es-salaam.
Juhudi za kumsaka kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ili
aweze kutoa taarifa ya tukio hilo,hazikufanikiwa.Baada ya kudaiwa kuwa mkuu
huyo yupo nje ya ofisi kikazi yeye na msaidizi wake.
0 Comments