SINGIDA | 05 Juni 2025 –
Afisa Elimu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Elipidius
Baganda, pamoja na wenzake wanne, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya
Singida wakikabiliwa na tuhuma za utakatishaji wa zaidi ya shilingi milioni 44.
Kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka wa
Serikali, Marshal Mseja, aliyesoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi
Mfawidhi Fadhil Luvinga, fedha hizo zilipaswa kutumika kwa shughuli za michezo
ya shule za msingi kupitia mashindano ya UMITASHUMTA mwaka 2023. Hata hivyo,
Dkt. Baganda anadaiwa kuzitumia kwa maslahi binafsi.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni
Evance Mlongo (mwalimu wa Shule ya Sekondari Mughanga), Paschal Kichambati
(mkuu wa Shule ya Sekondari Mghanga), James Lazaro (Afisa Elimu Maalum,
Manispaa ya Singida) na Deonatus Malima (Afisa Fedha, Manispaa ya Singida).
Watatu wa mwisho wanashtakiwa kwa kutoa msaada katika kutekeleza kosa hilo.
Kwa sasa, Dkt. Baganda amenyimwa
dhamana kutokana na uzito wa tuhuma dhidi yake na amepelekwa rumande. Mwalimu
Evance Mlongo pia ameshindwa kutimiza masharti ya dhamana na amepelekwa
rumande. Hata hivyo, washtakiwa wengine watatu wamefanikiwa kupata dhamana.
Kesi hiyo imepangwa kuendelea
kusikilizwa tarehe 18 Juni 2025.
0 Comments