MIRADI YA MAENDELEO SANZA MANYONI





Serikali imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini ikiwemo miradi ya Afya ambayo imewasaidia wananchi kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya afya.

Hayo yamesemwa na mtendaji wa kijiji cha Ntopo kata ya Sanza Wilaya ya Manyoni  Mkoani Singida Dominic Ulaya mbele ya kamati ya siasa Mkoa ambayo ipo kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kupitia ilani ya Chama cha mapinduzi CCM.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi katika kata hiyo Ulaya amesema pamoja na miradi mingine wamejenga kituo cha afya kimoja na zahanati mbili ambapo kituo cha afya kimeanza kufanya kazi kwa kuwahudumia wagonjwa wan je.

Amesema miradi  mingine ni ya elimu na mawasiliano huku akieleza baadhi ya changamoto zinazowakabili katika shughuli za utekelezaji wa miradi hiyo kuwa ni upungufu wa watumishi katika kada zote, madawati na vyumba vya madarasa pamoja na ofisi ya afisa mtendaji wa kata.

Hata hivyo mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Singida Martha Mlata amewaagiza wananchi kupanda miti kuzunguka kituo hicho cha afya na kufanya usafi ili kuweka mazingira katika hali ya usalama.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments