RASTA SINGIDA NA DODOMA WAMUENZI BOB MARLEY KWA KUPANDA MITI 200 NA KUTOA MSAADA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI

 








Mwenyekiti wa eneo hilo akikabidhiwa miti na madaftari ya wanafunzi na kwaajiri ya kupanda katika maeneo yao na Mratibu wa maandalizi Ninah Alute
 







           Mwanafunzo Shafiih Shaban akitoa neno la shukrani kwaniaba ya wanafunzi

SINGIDA

Katika kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha nguli wa muziki wa Reggae duniani, Robert Nesta Marley maarufu kama Bob Marley, Umoja wa Rasta wa mikoa ya Singida na Dodoma waliungana kwa pamoja kumuenzi kwa vitendo vya upendo na mazingira.

Tarehe 11 Mei ya kila mwaka huwa ni siku maalum ya kumkumbuka Bob Marley na mchango wake kwa jamii kupitia muziki na ujumbe wa haki, upendo na amani. Mwaka huu, wafuasi wa Rastafari walimuenzi kwa kupanda miti zaidi ya 200 katika Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida.

Mbali na hilo, walitembelea Shule ya Msingi Ikungi, ambayo ni shule ya bweni kwa watoto wenye mahitaji maalum, na kuwapatia msaada wa madaftari zaidi ya 100, kalamu, na chakula, ikiwa ni ishara ya upendo na mshikamano wa kijamii.

Wakiwa katika Kata ya Puma, Rasta hao waligawa miche ya miti ya aina mbalimbali, ikiwemo ya matunda, kwa wakazi wa maeneo hayo. Pia walitoa elimu kuhusu umuhimu wa upandaji miti na utunzaji wa mazingira, wakisisitiza kuwa mazingira bora ni urithi wa vizazi vijavyo.

Katika Kata ya Ikungi, walipanda miti zaidi ya 150 kwenye maeneo mbalimbali ya jamii na shuleni. Akimwakilisha Mbunge wa Jimbo la Ikungi, Mhe. Miraji Mtaturu, ambaye alikuwa bungeni Dodoma, Makamu Mkuu wa Shule ya Msingi Ikungi, Mwalimu Juma Mpinda, aliwashukuru na kuwapongeza Rasta hao kwa moyo wao wa uzalendo na kujitolea kwa ajili ya watoto na mazingira.

“Hii ni hatua nzuri ya kuigwa. Tunawashukuru kwa moyo wenu wa upendo kwa jamii na kwa kuthamini watoto wetu,” alisema Mwl. Mpinda.


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments