Na Cales katemana Singida
Mashindano ya Mei Mosi 2025 yameendelea kuwasha moto mkoani Singida, ambapo timu za Wizara ya Uchukuzi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) zimefuzu kwa kishindo hatua ya fainali ya mchezo wa kuvuta kamba kwa wanaume na wanawake.
Katika mchezo wa nusu fainali ya wanaume uliopigwa kwenye Uwanja wa Magereza, timu ya Wizara ya Uchukuzi iliibuka na ushindi wa mivuto 2-0 dhidi ya Ofisi ya Rais – Ikulu. Mchezo huo uliwavutia mashabiki wengi kutokana na ushindani mkali na mbinu za hali ya juu zilizotumika.
Kwa upande wa wanawake, timu ya TAKUKURU ilionesha uwezo mkubwa kwa kuwashinda Wizara ya Mambo ya Ndani kwa mivuto 2-0, na hivyo kufuzu fainali kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano haya.
Katika michezo mingine ya nusu fainali, timu ya Wizara ya Maliasili na Utalii (wanaume) iliibuka na ushindi wa mivuto 2-0 dhidi ya Wizara ya Mambo ya Ndani, huku timu ya wanawake ya Wizara ya Uchukuzi ikiibuka na ushindi wa mivuto 2-0 dhidi ya Wizara ya Afya.
Kwa
sasa, fainali ya wanaume itawakutanisha Wizara ya Uchukuzi dhidi ya Wizara ya
Maliasili na Utalii, huku fainali ya wanawake ikizikutanisha TAKUKURU na Wizara
ya Uchukuzi. Mashindano haya yamekuwa na mvuto mkubwa, yakionesha kuimarika kwa
viwango vya ushindani na ushiriki wa taasisi mbalimbali za serikali.
0 Comments