SINGIDA
Meya wa Manispaa ya Singida, Mhe. Yagi
Kiaratu, amesema kuwa changamoto nyingi zinazoikabili manispaa hiyo
zinasababishwa na uzembe na mapungufu ya baadhi ya watendaji wa Halmashauri.
Akizungumza katika kikao cha robo ya
tatu kilichofanyika katika ukumbi wa VETA, mjini Singida, Mhe. Kiaratu
alimhimiza Mkurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha anashughulikia kero za
wananchi kwa wakati, ili kuondoa malalamiko yasiyo ya lazima.
"Tunataka kuona hatua za haraka
zinachukuliwa kila mara panapojitokeza changamoto katika maeneo yetu. Wananchi
wanahitaji huduma bora na majibu ya haraka," alisema Mhe. Kiaratu.
Aidha, Mhe. Kiaratu ametoa wito kwa
wananchi kushiriki kikamilifu katika vikao na shughuli za maendeleo ili kutoa
maoni na mchango wao katika kuboresha huduma za jamii.
Kwa upande wao, Naibu Meya wa Manispaa
ya Singida, Mhe. Mbua Chima, na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Singida Mjini,
Bi. Luciya Mwiru, wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo katika Manispaa hiyo.
"Rais wetu ameendelea kutujali
kwa kutuletea fedha za miradi ya afya, elimu na miundombinu. Tunapaswa
kuzitumia vizuri kwa manufaa ya wananchi," walisema wajumbe hao.
0 Comments