Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Singida Bi Zulfat Muja akiongea na viongozi mbalimbali wa chama baada ya mapokezi
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Bi Lucy Boniphace Shehe akiongea jambo na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Singida Zulfat(kulia) Muja baada ya kusaini kitabu cha CCM Mkoa Singida
Baada ya Mapokezi kazi imeanza ya kutembelea miradi ya UVCCM katika Stend ya Vumbi kiwa ni mradi wa maduka katika manispaa ya Singida.
Singida17.03.2025
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida, Zulfat Muja, amepokelewa rasmi katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Singida baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo. Mapokezi hayo yaliongozwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Lucy Shee, pamoja na Katibu Mwenezi wa Mkoa wa Singida, wakimkaribisha kwa heshima na pongezi kwa ushindi wake.
Baada ya mapokezi hayo, Zulfat Muja alipata fursa ya kuzungumza na viongozi mbalimbali wa chama ndani ya ofisi hizo, ambapo alitoa wito kwa vijana wa UVCCM kuachana na makundi yaliyokuwepo wakati wa uchaguzi. Alihimiza mshikamano, akisisitiza kuwa sasa ni wakati wa kuwa na kundi moja lenye umoja kwa lengo la kuimarisha maendeleo ya jumuiya hiyo na chama kwa ujumla.
“Nawaomba
vijana wote wa UVCCM Mkoa wa Singida tusahau tofauti zetu za uchaguzi na sasa
tushikamane kama familia moja. Umoja wetu ndio nguzo imara ya chama chetu cha
Mapinduzi, na maendeleo ya UVCCM yatatokana na mshikamano wetu,” alisema Zulfat
Muja.
0 Comments