Sajad Haider akiongea na Mayatima na wjane baada ya kukabidhi futari mjini Singida.
Mkurugenzi wa Biosustain Sajad Haider akitoa futari katika msikiti wa Mwankoko kata ya Mwankoko manispaa ya Singida.
Singida
15.03.2025
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Pamba cha Biosustain, Sajad Haider, ametoa msaada wa futari kwa wajane na yatima katika Kata ya Mughanga, Manispaa ya Singida. Akizungumza baada ya kukabidhi futari hiyo, Haider alisema kuwa kiwanda hicho kimekuwa na utaratibu wa kusaidia jamii kila mwaka, hususan katika kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Wanufaika wa futari hiyo, Bi Kashinde Kawili na yatima Natharati Ismail, walimshukuru Mkurugenzi huyo kwa moyo wake wa kujitolea kuwasaidia watu wenye maisha magumu. Kwa upande wake, Amirat Jai wa Mkoa wa Singida, Bi Aisha Ramadhani, aliwataka kinamama hao kutokata tamaa na maisha licha ya kuondokewa na waume zao. Pia, alimsifu Sajad Haider kwa juhudi zake za kusaidia jamii katika maeneo mbalimbali.
Kampuni ya
Biosustain leo imegawa msaada wa futari katika kata mbili; Kata ya Mughanga kwa
wajane na yatima, na Kata ya Mwankoko kwa wazee wasiojiweza katika Msikiti wa
Mwankoko.
0 Comments