SAFARI YA MAGIC PRESSURE KUELEKEA KIGOMA YAIVA

 

Katibu wa Mabinwa wa Mkoa wa Singida Magic Pressure Abuu Juma akiongea na wanahabri katika ukumbi wa chama cha Soka Mkoa wa Singida SIREFA.

Mwenyekiti wa Magic Pressure Abdala Kawaka akifungua mkutano huo.

Mwenykiti wa chama cha soka mkoa wa Singida SIREFA Hamisi Kitila akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.


katikati ni Mkurugenzi wa Biosustain akionga na waandishi wa Habari baada ya kuchagia fedha kwaajiri ya maandalizi ya safari ya Kigoma.


Mwenyekiti wa timu ya Singida Veteran Edwin Christopher akisikiliza mkutano wa maandalizi ya timu ya Magic Pressure kuelelea kigoma.


Na Mwandishi Wetu

Maandalizi ya kuelekea Ligi ya Mabingwa wa Mikoa nchini, inayotarajiwa kuanza tarehe 13 Machi 2025 katika kituo cha Kigoma, yameanza rasmi kwa Bingwa wa Mkoa wa Singida, timu ya Magic Pressure, kuanza kupokea michango mbalimbali kutoka kwa wadau wa soka.

Uongozi wa timu hiyo umezungumza na wanahabari wa mkoa wa Singida kuhusu maandalizi yao, huku wakipokea msaada muhimu kutoka kwa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Pamba cha Biosustain, Sajad Haider.

Akizungumzia maandalizi hayo, Katibu wa Magic Pressure, Abuu Juma, amesema kuwa timu yao ipo tayari kwa mashindano hayo, kimwili, kiufundi na kiakili, huku wakitambua ushindani mkubwa kwani kila timu inapigania kusonga mbele katika hatua inayofuata.

Kwa upande wake, Sajad Haider, kama mmoja wa wadau wa soka mkoani hapa, ametoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kuichangia timu hiyo ili iweze kushiriki kikamilifu katika mashindano hayo. Aidha, ameonyesha dhamira yake ya kusaidia maendeleo ya soka kwa kuchangia shilingi milioni moja na nusu kwa timu ya Magic Pressure.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida, Hamisi Kitila, amepongeza juhudi za Magic Pressure na kueleza kuwa mkoa una dhamira ya kuhakikisha Singida inakuwa na timu nyingine zinazoshiriki ligi za madaraja ya chini, mbali na Singida Black Stars, ili kuongeza ushindani na kukuza vipaji vya wachezaji chipukizi.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments