Mkuu wa taasisi ya kuzuiya na kupambana na Rushwa Mkoa wa Singida Sipha Mwanjala akifungua semina hiyo iliyoandaliwa na Takukuru.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego akiongea na Viongozi wa dini na wazee wa kimila,viongozi mabalimbali wa taasisi na wazee maalufu n.k
Mwezeshaji wa Semina hiyo ya Sikumoja kutoka Takukuru mkoa Singida akitoa mada kwa washiriki wa Semina hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Singida akiongea na msanii wa maarufu wa mashairi mkoa wa Singida Mussa Mshairi.
Singida
Viongozi wa dini na wazee wa kimila wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya rushwa, wakisisitizwa kuwa rushwa siyo tu kosa la kisheria bali pia ni kinyume na maadili ya imani mbalimbali.
Wito huu umetolewa katika semina
maalum iliyoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
Mkoa wa Singida, ikilenga kuwawezesha viongozi wa dini, wazee wa kimila, na
viongozi wa taasisi mbalimbali kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya
rushwa.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida, Sipha
Mwanjala, amesisitiza kuwa rushwa inakwamisha maendeleo kwa kusababisha miradi
kutotekelezwa ipasavyo, hali inayowanyima wananchi huduma muhimu walizostahili.
Pia, ameeleza kuwa rushwa huchochea vitendo vingine vya kihalifu kama vile
wizi, unyanyasaji wa kijinsia, na ukiukwaji wa haki za binadamu, hivyo kudhoofisha
mshikamano wa jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima
Dendego, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika semina hiyo, amewahimiza wananchi
kushiriki kikamilifu katika kupambana na rushwa, hasa wakati huu ambapo nchi
inakaribia kipindi cha uchaguzi. Amewataka viongozi wa dini na wazee wa kimila
kuendelea kuhamasisha uadilifu na uwajibikaji ndani ya jamii.
Washiriki wa semina hiyo, wakiwemo
Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Singida, Ally Ommary Nuna, na mzee maarufu Joseph
Sabole, wameeleza kuwa rushwa inahatarisha utulivu wa nchi kwa kusababisha
mgawanyiko na kukwamisha maendeleo. Wamependekeza kuwa mafunzo kama haya
yaendelee kushirikisha vyombo vya ulinzi na usalama ili kuwezesha mikakati
madhubuti ya kupambana na tatizo hilo.
0 Comments