CCM KATA YA KINDAI YAADHIMISHA MIAKA 48 KWA UPANDAJI MITI NA USAFI WA MAZINGIRA

 

Mwenyekiti wa CCM kata ya Kindai Iddi Ommary Munda akiongea na wananchi na viongozi wa CCM kata ya Kindai baada ya Kufanya shughuli za maendeleo ikiwamo upandaji Miti.

Diwani wa kata ya kindai Mhe,Ommary Salum akiongea mazuri yaliyofanyika katika maendeleo ya kata ya Kindai Manispaa ya Singida.

kazi ya upandaji miti ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM kata ya Kindai Iddi Munda.

Diwani wa kata ya kindai Mhe,Ommary Salum akishiriki katika zoezi la kuhakikisha upandaji miti katika maeneo mbalimbali ya kata hiyo. 




SINGIDA

Katika kuelekea maadhimisho ya kutimiza miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kitaifa, CCM Kata ya Kindai, Manispaa ya Singida, imeadhimisha siku hiyo kwa kufanya shughuli za upandaji miti na usafi wa mazingira.

Maadhimisho hayo yameongozwa na Diwani wa Kata ya Kindai, Mhe. Omarry Salum, pamoja na Mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo, Ndg. Idi Munda. Viongozi mbalimbali wa chama na wanachama wa CCM kutoka kata hiyo walishiriki kwa pamoja katika shughuli hizo, wakionyesha mshikamano na uzalendo kwa jamii yao.

Akizungumza baada ya tukio hilo, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kindai, Ndg. Idi Munda, aliwapongeza wanachama kwa kuendelea kukiunga mkono Chama cha Mapinduzi na jumuiya zake chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Alisisitiza kuwa Rais Samia ameendelea kuenzi misingi iliyoasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, huku akidumisha amani na utulivu wa nchi.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Kindai, Mhe. Omarry Salum, alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa vitendo, hususan katika kuendelea kuleta fedha kwa ajili ya maendeleo ya Manispaa ya Singida na Kata ya Kindai. Alibainisha kuwa fedha hizo zimewezesha ujenzi wa madarasa ya shule za msingi na sekondari, kuboresha huduma za afya, pamoja na kuimarisha miundombinu ya kata hiyo.

Aidha, Diwani huyo aliunga mkono maamuzi ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kwa kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa nafasi ya Urais, pamoja na mgombea mwenza wake na Rais wa Zanzibar, ikiwa ni hatua muhimu ya kuendelea kuimarisha maendeleo ya nchi yetu.

#CCM48 #Singida #Kindai #MaendeleoKwaVitendo

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments