Ni kikao kazi cha Taasisi za Dini ya Kiislam Mkoa wa Singida na Ofisi ya Shekh wa Mkoa wa Singida.
Na Mwandishi Wetu
Ofisi ya
Sheikh wa Mkoa wa Singida, chini ya BAKWATA na uongozi wa Sheikh wa Mkoa,
Sheikh Issa Nassor, pamoja na Katibu wa BAKWATA mkoa, Ommary Ally Muna,
imekutana na viongozi wa taasisi za Kiislamu mkoani Singida kwa ajili ya
kujadili mikakati ya maendeleo ya taasisi hizo.
Mkutano huo
umejikita katika kujenga ushirikiano wa pamoja kwa lengo la kukuza maadili ya
Kiislamu, kuimarisha miongozo ya dini, na kushirikiana katika kubuni miradi ya
maendeleo hususan katika sekta za elimu, afya, na mambo mengine ya kijamii kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali.
Sheikh Nassor amesisitiza kuwa mshikamano wa taasisi hizo ni nguzo muhimu katika kuleta maendeleo endelevu ndani ya jamii ya Kiislamu mkoani Singida.
#BAKWATASingida
#Maendeleo #UmojaNaMaadili #Malundeblog#matukio daima
0 Comments