Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa
Viti Maalum Mkoa wa Singida, Mhe. Martha Gwau, amezindua rasmi ujenzi wa nyumba
ya mtumishi wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) mkoani Singida kwa kuchangia
vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3.3. Vifaa hivyo
ni pamoja na matofali, saruji, mchanga pamoja na kugharamia mafundi wa ujenzi
huo.
Mradi huo
unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Februari. Akizungumza wakati wa
makabidhiano ya msaada huo, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Singida, Bi. Martha
Kayaga, amempongeza Mhe. Gwau kwa mchango wake katika hatua ya awali ya ujenzi
huo.
Aidha,
ametoa wito kwa wadau wengine kushiriki katika kufanikisha mradi huo ili
ukamilike kwa wakati na kuwanufaisha wanachama wa UWT mkoani Singida.
0 Comments