Picha na matukio mbalimbali ya ziara ya Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe akiwa katika ziara mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Godwin Gondwe akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego katika Ziara hiyo.
Mkurugenzi wa kiwanda cha Pamba BioSustain Tanzania Ltd Dr Haiher Riyaz akimtembeza Waziri Kigahe Katika kiwanda hicho.
Naibu Waziri Kigahe akiwa katika kiwanda cha kusindika mafuta ya Alizet cha Mount Meru mjini Singida.
Naibu Waziri akiwa katika kiwanda kipya cha kisasa cha Kusindika Mafuta ya Alizet Wild Flower Granis&oil Mills
Na Mwandishi Wetu
Singida Tanzania
Wamiliki wa viwanda mkoani Singida wameiomba serikali kutatua tatizo la ukatikaji wa umeme katika njia za usambazaji wa nishati hiyo, jambo ambalo limekuwa likiathiri uzalishaji katika viwanda vyao.
Wakizungumza na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe, wakati wa ziara yake ya kutembelea viwanda mbalimbali mkoani Singida, wamiliki hao walitoa wito kwa serikali kuhakikisha changamoto hiyo inatatuliwa haraka ili kuboresha mazingira ya uzalishaji.
Akijibu malalamiko hayo katika ziara yake kwenye viwanda vya Mount Meru, Wild Flower Grains & Oil Mills, na BioSustain Tanzania Ltd, Mhe. Kigahe alisema kuwa suala la upatikanaji wa umeme limeshughulikiwa kwa kiasi kikubwa kupitia Mradi wa Mwalimu Nyerere, ambao umekamilika na utaimarisha upatikanaji wa nishati hiyo. Aidha, aliagiza uongozi wa mkoa wa Singida kuhakikisha tatizo la umeme linafanyiwa kazi kwa haraka.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya
Singida, Mhe. Godwin Gondwe, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida,
Mhe. Halima Dendego, alisema kuwa Mkuu wa Mkoa ameagiza Meneja wa TANESCO Mkoa
wa Singida kuhakikisha anatoa taarifa rasmi juu ya tatizo hilo ndani ya siku
tatu.
0 Comments