NAIBU WAZIRI WA VIWAMDA NA BIASHARA MHE,EXAUD KIGAHE AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI SINGIDA



 




Na Mwandishi Wetu

Singida, Tanzania – 

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaudi Kigahe, ameanza ziara ya siku tatu mkoani Singida kwa kutembelea viwanda mbalimbali pamoja na machimbo ya dhahabu katika mgodi wa Shanta Gold Mine Limited wilayani Ikungi. Ziara hiyo inalenga kutathmini maendeleo ya sekta ya viwanda na madini, pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili wawekezaji na wazalishaji.

Akiwa katika machimbo ya dhahabu ya Shanta Gold Mine, Mhe. Kigahe alisikiliza changamoto mbalimbali zinazoikabili machimbo hayo, ikiwemo tatizo la ukatizaji wa umeme mara kwa mara, hali inayosababisha ucheleweshaji wa uzalishaji na kuongeza gharama za uendeshaji. Pia, alielezwa kuhusu changamoto za miundombinu ya barabara, ambazo zimeathiri upatikanaji rahisi wa vifaa na usafirishaji wa madini kutoka mgodini.

Aidha, Naibu Waziri alipokea malalamiko kuhusu baadhi ya wananchi wanaogomea kupisha maeneo ambayo tayari mgodi umekamilisha malipo ya fidia kwa ajili ya shughuli za uchimbaji. Aliwataka wananchi kushirikiana na wawekezaji kwa kuheshimu makubaliano ya fidia ili kuwezesha maendeleo ya sekta ya madini na kuinua uchumi wa eneo hilo.

Ziara ya Mhe. ExaudKigahe inatarajiwa kuendelea kesho kwa kutembelea viwanda vingine, ikiwemo Kiwanda cha Mount Meru, ambacho kinajishughulisha na usindikaji wa mafuta ya alizeti. Aidha, atakutana na wadau wa sekta ya viwanda na biashara ili kujadili fursa na changamoto zinazohitaji ufumbuzi wa haraka katika sekta hiyo. 







Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments