Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego akitolea ufafanuzi namna fedha za makusanyo hayo zitakavyo patikana.
Dkt Gibance Kayuni akitolea ufafanuzi juu ya madeni ya mapato ya mauzo ya mifugo zinavyo kuwa na malimbikizo baada ya kubaini deni la mkoa wa Singida.
Wenyeviti wa Halnashauri (kushoto) ni Mhe,Ally Mwanga Ikungi katikati ni mwenyekiti wa Halmshauri ya Itigi Mhe Hussein Simba na Mhe Elia Digha Wilaya ya Singida wakisikiliza kwa makini taarifa ya Wizara ya Mifugo.
Kushoto ni Suleiman Mwenda mkuu wa wilaya ya Iramba na Mkuu wa wilaya ya Ikungi Thomas Apson wakiwa katika kikao kazi hicho.
Singida
Wizara ya Mifugo
imezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha zinalipa malimbikizo ya madeni
yanayotokana na makusanyo ya mapato ya mifugo, kufuatia kuwepo kwa madeni hayo
kwa muda mrefu.
Akizungumza
katika kikao maalum kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida,
kiongozi wa tume maalum kutoka Wizara ya Kilimo, Dkt. Gibonce Kayuni,
alisema kuwa Singida ni miongoni mwa mikoa yenye madeni ya mirahaba hiyo.
Alifafanua kuwa deni la mkoa wa Singida ni shilingi milioni 622, huku fedha
zilizo lipwa hadi sasa zikiwa ni milioni 550 pekee.
Mtaalamu wa fedha
kutoka Wizara ya Fedha aliyeambatana na tume hiyo, Abdala Rachi, alisema
kuwa hadi sasa wamefanikiwa kukusanya asilimia 12 ya fedha hizo. Aidha, Mkuu wa
Mkoa wa Singida ameahidi kuhakikisha kuwa fedha hizo zinalipwa ifikapo mwishoni
mwa mwezi huu.
Kwa upande wake, Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, alisema kuwa mkoa unaendelea kufuatilia
makusanyo kutoka kwa halmashauri mbalimbali ili kuhakikisha deni hilo linalipwa
kwa wakati, licha ya changamoto zilizopo.
Kikao hicho
kiliudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wenyeviti wa
Halmashauri, pamoja na Wakuu wa Idara kutoka halmashauri zote za mkoa wa
Singida.
0 Comments