WANAHABARI JIFUNZENI LUGHA ZA KIGENI ILI KUONGEZA UFANISI .

 


Anne Makinda kamisaa wa Sensa Tanzania Bara na Spika wa Bunge la Jamihuri ya Muungano wa Tanzania akiongea na wanahabari kutoka mikoa ya Dodoma na Singida katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini Saidi Amiri akiongea na washiriki katika semina hiyo mjini Singida.





Mfunzo haya ya Siku mbili yamewakutanisha wanachama wa klabu za waandishi wa Habari kutoka mikoa ya Dodoma na Singida.


Singida

Namwandishi wetu

Waandishi wa habari wametakiwa kujifunza lugha za kigeni na kujisomea maandiko mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika kazi zao, hususan wakati wa kuripoti taarifa zinapohusu wageni kutoka nje ya nchi

Wito huo umetolewa na Kamisaa wa Sensa Tanzania Bara, ambaye pia ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, wakati akifunga mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu usambazaji na matumizi ya matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022. Mafunzo hayo yaliwahusisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Dodoma na Singida.

Makinda amewataka waandishi wa habari kuwa wabunifu na kujiongeza katika taaluma yao kwa kuwa wao ndio kiungo muhimu cha kusambaza taarifa kwa jamii. Pia amewahakikishia kuwa hakuna mwandishi atakayekumbwa na matatizo endapo ataandika habari za uchunguzi kwa kufuata ukweli na usahihi.

Kwa upande wake, Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Mdoka Omary, amesema kuwa asilimia 15 ya watu wote duniani, ambayo ni zaidi ya bilioni moja, ni watu wenye ulemavu, huku wengi wao wakiwa wanawake.

Ameeleza kuwa sababu kuu za ulemavu ni pamoja na aina ya ulaji unaosababisha maradhi mapya, vita, umri wa kuishi, pamoja na ulemavu wa kuzaliwa nao.

 

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments