Naibu
Waziri anayeshughulikia Elimu Mhe. Zainab Katimba amesema Serikali imekuja na
Mpango wa Shule Salama kwa shule za Msingi na Sekondari ambao ni shirikishi na
jamaii ili kudhibiti mdondoko wa wanafunzi.
Mhe. Katimba ameyasema hayo wakati akifunga
mafunzo kwa Wenyeviti wa Bodi za Shule za Sekondari, Maafisa Maendeleo ya Jamii
ngazi ya Kata pamoja Maafisa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii ngazi ya
Mkoa kuhusu Mpango wa Shule Salama na Usimamizi wa Usalama wa Jamii katika chuo
cha Patandi mkoani Arusha leo tarehe 18.08.2024.
Amesema Serikali imekwishafanya jitihada za
kudhibiti mdondoko wa wanafunzi ikiwa ni pamoja kutoa Elimu bila Ada ili
kupunguza vikwazo katika uandikishaji wa wanafunzi, kujenga shule za Msingi na
Sekondari karibu na makazi ya wananchi ili kupunguza adha kwa wanafunzi
kutembea umbali mrefu, Kuimarisha mifumo ya utambuzi wa wanafunzi ambao wapo
kwenye hatari ya kuacha shule, Kuimarisha utaoaji wa huduma na ushauri na
unasihi pamoja na Kuandaa Mwongozo wa kuwarejesha Shule Wanafunzi walioacha
Shule.
Mhe. Katimba ameongeza kuwa pamoja na jitihada
hizo changamoto ya mdondoko wa wanafunzi katika Shule za Msingi na Sekondari
haijakwisha kabisa na Kasi ya kupungua kwa idadi ya wanafunzi wanaocha shule
haijakwisha kabisa.
“Uchambuzi wa sababu za kutokwisha kwa mdondoko wa
wanafunzi unaonesha kuwa mazingira yasiyo salama kwa wanafunzi wakiwa shuleni
na wakati wa kwenda na kurudi shuleni yanachangia kwa kiasi kikubwa kutokushuka
kwa kiwango cha mdondoko wa wanafunzi”.
Ili kuweka mazingira ya shule yaliyosalama
Serikali iliona ni vyema kuja na mkakati mpya unaojulikana kama Mpango wa Shule
Salama katika Shule za Msingi na Sekondari nchini.
Serikali imedhamiria kuboresha mazingira ya
ufundishaji na ujifunzaji kwa Kuimarisha ushiriki wa wazazi/walezi na Jamii
katika kusimamia ufundishaji na ujifunzaji pamoja na mahudhurio ya wanafunzi’.
Kuimarisha mifumo ya kupokea na kushughulikia
malalamiko ya wanafunzi katika Elimu ya Msingi na Sekondari na
Kuimarisha utoaji wa huduma ya Chakula na Lishe
kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari.
0 Comments