Singida
23 Aug 2014
Monekano wa Baadhi ya majengo mapya ya Chuo cha Ualimu Dakawa ambapo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imetembelea na kumeridhishwa na Utekelezaji wa Mradi huo.
Majengo mapya ya 32 yanayojengwa katika chuo hicho yatawezesha Chuo kudahili Walimu tarajali 1000 ambapo ni ongezeko la wanafunzi 500 kutoka hali ilivyo sasa.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Musa Sima amekitaka Chuo hicho kutoa mafunzo kwa vitendo zaidi na kuagiza ujenzi ukamilike ili ifikapo 2025 waanze kutumia majengo hayo.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omar Kipanga akizungumza katika ziara hiyo amesema Chuo cha Ualimu Dakawa kimejikita katika mafuzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada mchepuo wa Sanaa, Lugha na Hisabati na ngazi ya cheti kwa Lugha ya Kingereza na kwamba mradi huo unahusisha ujenzi wa majengo 34 yanayojengwa kwa awamu mbili huku awamu ya kwanza ikiwa imefikia asilimia 98.
0 Comments