JELA MIEZI MITATU KWA KUKUTWA KWENYE ZIZI USIKU -IKUNGI

 


Ikungi

Namwandishi wetu

MAHAKAMA ya Mwanzo Sepuka Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida imemuhukumu Ayubu Rashidi (Mkila) (39) kwenda jela miezi mitatu baada ya kudaiwa kukutwa  ndani ya zizi la mifugo usiku bila idhini ya mwenye nyumba.

Mahakama imemkuta na hatia baada ya kutolewa maelezo juu ya kesi hiyo namba 95/2024 chini ya kifungu cha sheria namba 299 (9) jina sura 16 kanuni ya adhabu na hii ni baada ya kukiri mwenyewe kuwepo kwenye eneo hilo bila idhini ya wenye nyumba kwa mujibu wa hati ya mashtaka na maelezo ya mlalamikaji imethibitisha kitendo hicho.

Akitoa maelezo yake mshtakiwa mbele ya mahakama alikubali kosa na kukiri wazi pasipo shaka na kumuomba mlalamikaji amsamehe kwa kosa hilo na hatarudia  hii ni  baada ya kuulizwa na mahakama ikiwa ana kitu cha kujitetea.

Mahakama ya Sepuka ili mhukumu Ayubu Saidi Rashidi (39) kwenda jela miezi mitatu akatumike kifungo hicho na hudumu hiyo imesomwa mbele ya mlalamikaji na mshtakiwa katika mahakama ya wazi na haki nah ii baada ya mahakama kumuona mshtakiwa hana makosa mengine na hiyo ni mara ya kwanza kufikishwa polisi na mahakamani.

Hakimu mkazi wa mahakama ya mwanzo Sepuka Ys Zakaria alitoa hukumu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani na mlalamikaji wa kesi hiyo Muhidini Kasimu Njiku akidai kumkuta mtuhumiwa Ayubu akiwa ndani ya zizi la mbuzi wake bila idhini yake.

Akisoma hukumu hiyo tarehe 20 August 2024 hakimu mkazi Zakaria amesema katika taarifa yake kuwa mahakama yake imesikiliza maelezo kutoka kwa mlalamikaji kwamba alimkuta Ayubu aiwa ndani ya zizi la mbuzi wake usiku bila idhini yake hivyo mahakama imeridhika pasipo mashaka kuwa mshtakiwa ametenda kosa hilo kinyume na sheria hivyo mahakana imemtia hatiani.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliosomwa na PC Sadamu wa kituo cha Polisi Sepuka imesema mnamo tarehe 19 August 2024 muda usiojulikana usiku mshtakiwa Ayubu Rashidi (39) mkila aliingia kwenye nyumba ya Muhidini Kasimu Njiku wakati wamelala na familia yake hadi ndani ya zizi la mbuzi na kuingia ndani bila idhini hali akijua wazi kuwa hilo ni kosa.

Hati ya Mashtaka imesema muhidini alikwenda kwenye zizi la mbuzi baada ya kushtuka kelele za mifugo hiyo usiku huo na kutia shaka akamkuta mshtakiwa Ayubu akiwa ndani ya zizi la mbuzi bila idhini yake hivyo akatia shaka kuwa alikuwa ana nia ya kutaka kuiba mifugo yake.

Akizungumza na vyombo vya habari  kwa njia ya simu Mwenyekiti wa kitongozji cha kikundufe Petro Mtinangi amesema Ayubu alikuamatwa saa 11:00 asubuhi akiwa ndani ya zizi la mbuzi kwenye nyumba ya Asha Njolo na katika mahojianao na mkazi wake Mhidini Njiku alikiri kuwepo hapo bila idhini akidai alikuwa amelewa pombe.

Mwenyekiti Petro amesema familia ya nyumba hiyo ilizidi kumtia shaka na kuhoji kisa cha kuwepo ndani ya mifugo usiku huku akitoka jasho na wasiwasi mwingi akiwa karibu na mbogoma la mbuzi lenye thamani y ash 80,000/= wakahesabu mifugo yao wakaona iko sawa na alipohojiwa kilichomfanya awepo hapo usiku akawa mkali akaanza kufoka wakaamuza wapige mayowe.

Watu walipofika muda huo wakamhoji sana akadaaaaai alifika hapo usiku akiwa amelewa pombe akaona ajihifadhi hadi asubuhi aende zake maelezo yake na muonekano wake haukuwaridhisha wananchi viongozi wa Kijiji waliitwa na baadae akapelekwa kituo cha polisi Sepuka na mbuzi huyo na baadae mahakamni kujibu mashtaka yake.


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments