IDARA YA FEDHA HALMASHAURI YA IKUNGI KAGUENI (POS) ZINAPOPATA TATIZO.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na Diwani wa kata ya Irisya Mh Ally Mwanga akitoa wito kwa mkuu wa Idar ya fedha katika kikao cha Baraza la wilayani humo.


Madiwani kutoka kata mbalimbali za Puma Mh Joseph Mtaturu na  kata ya Mang'onyi Mh Innocent Makomelo wakifuatilia hoja mbalimbali katika kikao hicho.

        Mh Dure wa kata ya Mungaa akichangia hoja juu ya tatizo la  Point of Sales (POS)  

Diwani wa kata ya Ligwa Mh Gabriel Alphonce naye akitoa maoni yake juu ya (POS) vifaa vya ukusanyaji mapato.

SINGIDA

11.11.2023

Ofisi ya idara ya fedha halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida imeombwa kufanya ukarabati wa haraka wa machine za kukusanyia mapato Point Of Sales [POS] pindi zipatapo hitilafu ili kuepusha kusimama kwa zoezi la ukusanyaji.

Wakizungumza katika kikao cha baraza la madiwani diwani Gabriel Alphonce wa kata ya Lighwa  na Mh Dure wa kata ya Mungaa wameomba machine hizo kufanyiwa marekebisho ya haraka.

Madiwani hao wamesema kuharibika kwa mashine hizo kunarudisha nyuma zoezi la ukusanyaji wa mapato na hivyo kusababisha halmashauri kushindwa kufikia malengoya ukusanyaji wa mapato.

Aidha mwenyekiti wa halmashauri hiyo Ally Mwanga amewasisitiza madiwani hao kusimamia vizuri zoezi la mapato na kuongeza kuwa halmashauri inajipanga kuongeza mashine za kukusanyia ili kurahisisha zoezi la ukusanyaji.

Naye katibu tawala wilaya ya Ikungi Rashidi Rashidi akimwakilisha mkuu wa wilaya hiyo amewapongeza madiwani hao kwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na Kuwaagiza viongozi kuwahamasisha wananchi kutumia vyoo bora na kunawa mikono ili kujikinga na mlipuko wa homa ya kipindupindu.


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments