Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa hana tatizo na kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba licha ya kumwambia mchezaji huyo kwamba hatowahi tena kuwa nahodha wa klabu hiyo.
Mourinho alimwambia Pogba kwamba sio nahodha wa klabu hiyo kutokana na wasiwasi kuhusu tabia yake.
Mshindi wa kombe la dunia Pogba 25 aliambiwa kuhusu uamuzi huo kabla ya mechi ya siku ya Jumanne ya kombe la Carabao dhidi ya Derby.
Kabla ya mechi , Mourinho alisema: "wamepumzishwa . Nilimpumzisha Luke Shaw, Paul, Victor Lindelof, Antonio Valencia na David de Gea. Lazima nicheze na kikosi kizuri. "
Kufuatia sare ya 1-1 siku ya Jumamosi. Pogba alisema kwamba angetaka timu hiyo kushambulia mara kwa mara katika uwanja wa Old Trafford. Tuko nyumbani na tunafaa kucheza vizuri zaidi .
Pogba amabaye alijiunga tena na United kutoka Juventus kwa dau lililovunja rekodi mwaka 2016 , alikuwa akiwachwa nje msimu uliopita na kusema kwamba hafurahii kusalia Old Trafford.
0 Comments