Serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imetoa ufafanuzi kuwa Jumatatu Septemba 24, 2018 ni siku ya kazi kama kawaida.
Baada ya Rais Magufuli kutangaza siku 4 za maombolezo kufuatia ajali ya MV Nyerere iliyoua watu 166, kumekuwa na mkanganyiko kidogo kwa baadhi ya watu kudhani Jumatatu itakuwa ni mapumziko.
Baada ya Rais Magufuli kutangaza siku 4 za maombolezo kufuatia ajali ya MV Nyerere iliyoua watu 166, kumekuwa na mkanganyiko kidogo kwa baadhi ya watu kudhani Jumatatu itakuwa ni mapumziko.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Msigwa amesema Rais Magufuli alitangaza siku 4 za maombolezo na sio siku za Mapumziko.
Msigwa ameandika;"Napenda kutoa ufafanuzi kuwa Jumatatu tarehe 24 Septemba, 2018 ambayo ni siku ya mwisho ya maombolezo ya Kitaifa, itakuwa ni siku ya kazi kama kawaida. Mhe. Rais Magufuli ametangaza siku 4 za MAOMBOLEZO na sio MAPUMZIKO."
0 Comments