Mmoja ya vijana wa kikosi cha uhokoaji akisimulia baada ya kutoka ndani ya shima hilo ikiwa nikatika kusaka mihili hiyo. |
Mmoja ya msimamizi wa kamati ya maafa anayejulikana kwa jina la PigaBao akimpamaelezo naibu waziri juu ya zoezi la uokoajia linavyo endelea. |
Naibu waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akiongea na wachimbaji wa mgodi wa Sekenke wilayani Iramba Mkoani Singida. |
Sekenke IRAMBA Singida Julai,21,2018
NAIBU Waziri wa Madini,Bwana Stansilaus Nyongo amewaagiza
wachimbaji wadogo wa madini kuhakikishaa wanachimba kwa kufuata taratibu na
sheria za uchimbaji na kuangalia namna bora ya uchimbaji huo ili kuepusha
kutokea vifo vya nguvukazi ya taifa.
Naibu Waziri huyo amewataka wachimbaji hao kutambua kwamba miili
hiyo ni mali ya serikali na kwamba kunapotokea matukio ya watu kupoteza maisha
kwa vifo serikali hupata hasara kutokana na kupungua kwa wazalishajimali.
Akizungumza na wananchi pamoja na wachimbaji katika mgodi wa
Sekenke One waliofurika kumsikiliza alipokwenda kukagua shughuli za uokoaji wa
miili ya wachimbaji wawili waliofunikwa na kifusi ndani ya shimo namba 19 “C”
zinavyoendela,Waziri Nyongo ameridhishwa na zoezi hilo linavyoendelea ambalo
limeonyesha matumaini ya upatikanaji wa miili hiyo.
Aidha Naibu waziri huyo amesisitiza kwamba kutokana na jitihada
zilizoonyeshwa na waokoaji hao na hivyo kushawishika kuongeza siku za zoezi
hilo ambazo zilikuwa zikamilike leo jumamosi na kuongeza hadi siku ya jumatano
ijayo na kuonya kuwa endapo miili hiyo haitapatikana,mgodi huo utafungwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya maafa wilaya ya
Iramba,Bwana Edward Kurwa akitoa taarifa kwa Naibu waziri wa madini amesema
mpaka sasa wameshafanikiwa kupata vifaa walivyokuwa wakifanyiakazi,ikiwemo
pampu na madumu waliyokuwa wakitolea kifusi.
Naye mmoja wa waokoaji Bwana Limbu Daudi amesema mpaka sasa
wameshafikia mwisho wa shimo hilo mahali walipokuwa wakifanyiakazi wachimbaji
hao,na kwamba kwa kuwa eneo hilo linaonyesha lilikuwa na reli hivyo wameanza
kufukua.
0 Comments