Mwili wa mmoja wa wachimbaji aliyefariki kwa kuangukiwa na shimo ukiwa kwenye gari teyali kwa safari ya mazikoni mkoani Mara. |
Mkuu wa wilaya ya Iramba Emmanuel Luhaula akiwa na vingozi wa wachimbaji wadogo wa madini katika Hospital ya wilaya ya Kiomboi . |
Kutoka wilayani IRAMBA Julai,23,2018 Waombolezaji
MKUU wa wilaya ya Iramba,Mkoani
Singida,Bwana Emmanueli Luhahula amewaongoza waombolezaji wa wachimbaji wadogo
wa madini kuaga miili ya watu wawili waliopoteza maisha baada ya kufukiwa na
kifusi cha mgodi wa madini wa Sekenke One,uliopo wilayani Iramba Mkoani
Singida.
Akizungumza wakati wa kuaga miili
hiyo kwenye majengo ya Hospitali ya wilaya ya Iramba,Bwana Luhahula ambaye pia
ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ametoa wito kwa
wachimbaji hao kudumisha ushirikiano uliopo huku akimwagiza Kamishina wa madini
kanda ya kati kufuatilia watalaamu wa GST ili waweze kufika na kuonyesha ramani
ya eneo hilo.
Bwana Luhahula hata hivyo
ametumia fursa hiyo pia kuwaagiza wamiliki wote wa migodi,wakiwemno wakaguzi na
mafundi wahakikishe wanasimamia vizuri na wawe makini katika usimamizi wa
shughuli za uchimbaji.
Naye mmiliki wa shimo namba 49
“C” lililosababisha ajali na kuchangia vifo vya watu wawili,Bwana Robert
Wambura amebainisha kuwa siku ya tukio julai,06 saa 10:30 usiku amepigiwa simu
na msimamizi wa kazi kwamba ajali imetokea duarani na duara limeanguka.
Kwa upande wake Katibu wa Sekenke
One,Bwana Joseph Jumanne Mnemba amebainisha kuwa kutokana na matukio ya ajali
zinazosababisha vifo,wamelazimika kuunda kamati ya kudumu itakayokuwa
ikishughulikia matukio ya uokoaji.
0 Comments