Afisa wa Idara ya Uhamiaji ikitoa maelezo kwa mgeni mualikwa mkuu wa mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi kulia ni kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba .. |
Katikati ni hakimu mkazi mkoa wa Singida Joice Mack Mind |
Mgeni muarikwa Mkuu wa mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi akipata maelezo kutoka katika banda la shirika la SEMA Singida. |
Wakili wa kujitegemea Frances Kitope akisoma risala kwa niaba ya mawakili binafsi |
Mkuu wa mkoa katika Picha maalum na mahakimu na wafanyakazi wa mahakama |
Picha ya pamoja na mawakili na Paraligos |
Vyombo vyote inavyo husika na masuala ya kutoa haki vimeombwa kukaa na kubuni mbinu zitakazo weza kuwapatia haki watoto ambao kwa kiasi kukubwa wamekuwa waathirika wa vitendo vya unyanyasaji.
Akiongea wakati wa kuhitimisha maadhimisho ya wiki
ya kisheria mkoani Singida mkuu wa mkoa wa Singida dr, Rehema Nchimbi amesema
ilikuhakikisha watoto wanapata hakiyao lazima vyombo vya kutoa haki viungane pamoja ilikutokomeza vitendo hivyo.
Amesema watoto katika maeneo mbalimbali wameathirika
na vitendo vya unyanyasaji laki hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yao.
Dr,Chimbi amesema umefika wakati vyombo vyote
vinavyohusika na haki kuja na mpango mkakati wa kuwasaidia watoto hao .
Amesema katika mikakati yao wawahusishe wazazi ambao
wamekuwa chanzo kikubwa cha matatizo hayo na kuishirikisha jamii ilikutoa
taarifa dhidi ya vitendo hivyo.
Amesema lengo la kufanya hivyo ni kutaka kutokomeza
kabisa suala la unyanyasaji kwa watoto ndani ya mkoa wa Singida.
0 Comments