KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA YA SINGIDA YATEMBELEA KIWANDA CHA MOUNT MERU MILLERS MJINI SINGIDA

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Singida Bw Elias Tarimo akiongea na waandishi wa habari baada ya kutembelea kiwanda cha kusindika mafuta ya Alizeti cha Mount Meru Milles kilichopo mjini Singida ili kujionea utekelezaji wa maagizo ya naibu waziri wa Mazingira Kangi Lugora baada ya kukifunga mpaka yatakapo fanyika marekebisho ya miundo mbinu ya maji taka na bomba la moshi kiwandani hapo.

Bw Nelson Mwakabuta ni meneja uhusiano wa kiwanda cha Mount Meru amesema kuwa zoezi la ukarabati wa miundo mbinu linaendelea usiku na mchana ili kuakikisha kazi ya uzarishaji inaanza maramoja.
Moja ya malalamiko ya wakazi waishio kandokando ya kiwanda hicho ilikuwa ni moshi unaotoka pindi kiwanda hicho kinapokuwa katika uzarishaji.

Hayo ni maji taka ambayo utoka katika mfumo wa uzarishaji na kuifadhiwa katika bwawa maalumu.
Uchimbaji wa matenki ya akiba ya maji ya mvua unaendelea .




Eneo la Ndani ya kiwanda linavyoonekana baada ya mashine kuzimwa.


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments