Rais Mteule wa Marekani Donald Trump
amesema anataka kufuta ombi la ununuzi wa ndege mpya za Air Force One ambazo
hutumiwa na marais wa Marekani.
Wiki sita kabla yake kuingia madarakani, aliandika kwenye
Twitter: "Boeing wanaunda ndege mpya aina ya 747 Air Force One za kutumiwa
na marais siku zijazo, lakini gharama yake imezidi, zaidi ya $4 bilioni. Futa
oda hiyo!"
Serikali ya Marekani iliingia kwenye mkataba na kampuni ya
Boeing wa kuundwa kwa ndege mbili au zaidi za kuwabeba marais.
Ndege hizo zilitarajiwa kukamilika na kuanza kutumiwa mwaka
2024.
Hisa za kampuni hiyo ya ndege ya Boeing zilishuka kwa zaidi ya
1% baada ya ujumbe huo wa Trump kwenye Twitter, ingawa zilijikwamua baadaye
alasiri.
Bw Trump hatarajiwi kutumia ndege hizo mpya, iwapo hatashinda
uchaguzi wa muhula wa pili mwaka 2020.
0 Comments