KITALU CHA MBEGU BORA YA PAMBA UKM 08

Stanslaus Beatus Chiwali Kaimu katibu tawala msaidizi wa huduma za uchumi na uzarishaji mkoa wa singida
 Mkoa wa Singida kupitia kilimo cha mkataba kati ya kampuni ya BIOSUSTAIN na wakulia umetaeuliwa kuzalisha mbegu bora ya pamba aina ya UKM08, kampuni hiyi ya BIOSUSTAIN ndiyo iliyo teuliwa katika mpango huo wa serikali wa kuzarisha mbegu hiyo bora UKM08.

kupitia kwenye mpango huo wa kuzariza mbegu mkoa wa Singida umetengwa kuwa kitalu cha kuzalisha mbegu bora ya zao la pamba kwasabu mkoa unakiwango kidogo cha wadudu wanaoadhili zao la pamba ukilinganisha na mikoa mingine
mbegu ya UKM08

Dr Riyaz Haider Mkurugenzi wa BIOSUSTAIN TANZANIA LTD
Kiwanda cha kukoboa  pamba  cha ginnery kilichopo Singida mjini kinauwezo wa kuchambua pamba tani elfu 20 na kutoa ajira ya muda mlefu  kwa wafanyakazi ndani ya  mezi 9, ukitizama uwekezaji uliyowekwa singida ni tofauti na upatikanaji wa zao hivyo wakulima mkoani hapa wanatakiwa kulima zaidi pamba ili waweze kujikwamua kiuchumi huku serikali na mwekezaji BIOSUSTAIN na wadau wa zao hili wanatakiwa kutoa elimu kwa wakulima juu ya zao la pamba.


Singida ni mkoa uliyochaguliwa na serikali kulima zao la pamba kama mbegu huku kampuni ya BIOSUSTAIN ndiyo kampuni yenye kiwanda mkoani hapa.


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments